
Ancelotti kuondoka Real Madrid
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti ataondoka katika klabu hiyo ya Uhispania mwishoni mwa msimu huu na kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil.
Muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 65 ataanza rasmi kuinoa Brazil tarehe 26 Mei baada ya kumalizika kwa msimu wa La Liga.
Anaondoka Santiago Bernabeu kama mmoja wa mameneja wenye mafanikio zaidi wa klabu hiyo.
Ancelotti alishinda mataji 15 katika misimu miwili kama meneja wa Real na msimu uliopita aliiongoza Los Blancos kushinda Ligi ya Mabingwa na La Liga mara mbili.
Hata hivyo, kuondoka kwake Real kunakuja baada ya kichapo cha Jumapili cha El Clasico kuwaacha Real kwa pointi saba nyuma ya vinara Barcelona zikiwa zimesalia mechi tatu.
Ukiondoa kuanguka kwa Barcelona, matokeo hayo yalithibitisha kwamba Real itamaliza msimu bila kombe kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne.